1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SanaaMarekani

Mahakama yatupilia mbali kesi dhidi ya Alec Baldwin

13 Julai 2024

Mahakama nchini Marekani imemfutia kesi ya uhalifu iliyokuwa ikimkabili mcheza filamu wa Marekani Alec Baldwin.

Mcheza filamu wa Marekani Alec Baldwin
Kesi dhidi ya Alec Baldwin, mcheza filamu wa Hollywood imefutwa kutokana na changamoto za upande wa ushahidiPicha: Ramsay de Give/REUTERS

Jaji Mary Marlowe Sommer alikubaliana na ombi la mawakili wa Baldwin la kufuta kesi hiyo baada ya timu ya utetezi ya nyota huyo wa Hollywood kifunkuushutumu upande wa mashtaka huko Santa Fe kwa utovu wa nidhamu.

Kesi hiyo iliyoanza siku ya Jumanne ilijikita katika swali la ikiwa kisa hicho cha kumpiga risasi mwigizaji wa sinema Halyna Hutchins mnamo 2021 kilikuwa ni matokeo ya uzembe.

Uamuzi huo umeimaliza ghafla kesi hiyo ambayo tayari iliwahi kutupiliwa mbali.

Ikiwa angekutwa na kosa, Baldwin angekabiliwa na kifungo cha miezi 18 jela.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW