Sheria na HakiUjerumani
Kesi dhidi ya mshukiwa wa mauaji Ujerumani yaanza
24 Oktoba 2023Matangazo
Mshukiwa huyo, mhamiaji kutoka Syria, ameshtakiwa kwa mauaji na anakabiliwa na mashitaka matatu ya majaribio ya kuua.
Waendesha mashitaka wa shirikisho katika mahakama ya juu ya Dusseldof wamewasilisha hoja wakisema mashambulizi hayo ya kisu yalichochewa na msimamo wa kidini.
Waendesha mashitaka pia wamesema mshukiwa anajiona kama shahidi wa kundi la kigaidi linalojiita dola la kiislamu, akipania kuua watu wengi kadri inavyowezekana. Mahakama ya Dusseldorf imepanga siku 18 za kusikilizwa kwa kesi hiyo hadi Januari 2024.