Kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta yaahirishwa
24 Januari 2014Hatua hiyo imechukuliwa na mahakama hiyo kufuatia ombi la mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda la kutaka muda zaidi wa kujipanga katika suala la mashahidi wake.Mahakama hiyo imesema badala yake siku hiyo ya Tarehe 5 Februari kutafanyika kikao maalum kitakachowahusisha washiriki wote wanaohusiana na kesi hiyo.kikao ambacho upande wa utetezi wa Uhuru Kenyatta unatarajiwa kutoa pendekezo la kutaka kesi hiyo ifutiliwe mbali.
Ili kufahamu ni vipi uamuzi huo wa ICC ulivyopokelewa nchini Kenya na waathirika wa machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008, Saumu Mwasimba amezungumza na Patrick Muchiri ambaye ni mwakilishi wa waathiriwa hao katika eneo la Bonde la Ufa. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hpo chini.
Mwandishi:Saumu Mwasimba
Mhariri:Abdulrahman Mohammed