1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi dhidi ya Yar´Adua yatupiliwa mbali- Nigeria

Eric Kalume Ponda12 Desemba 2008

Mahakama kuu nchini Nigeria imetupilia mbali kesi iliyowasilishwa na upande wa upinzani kupinga kuchaguliwa kwa rais wa Umaru Yar`Adua na kuondolea mbali hofu ya kuzuka kwa machafuko ya kisiasa nchini humo.

Kiongozi wa upinzani Muhammadu Buhari aliyewasilisha kesi.Picha: AP


Uamuzi huo pia unampa nafasi rais huyo huyo kuendelea kuliongoza taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Africa.


Wapinzani wakuu wa rais Yar`Adua pamoja na wachunguzi wengine wa kigeni, walidai uchaguzi wa mwaka wa 2007 uliomweka madarakani Rais Yar´Adua ulikumbwa na udanganyifu.


Akitoa uamuzi huo jaji Niki Tobi alisema kuwa wapinzani hao ambao ni kiongozi wa zamani wa kijeshi nchini humo Muhammadu Buhari na makamu wa rais wa zamani Atiku Abubakar, hawakuwa na ushahidi wa kutosha kuhusiana na madai hayo ya udanganyifu wakati wa uchaguzi huo mkuu


Wawili hao walikuwa wapinzani wakuu wa rais YarAdua wakati wa uchaguzi huo ambao ulikuwa wa kwanza kwa viongozi wa utawala wa kiraia kupokezana madaraka katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta.


Endapo mahakama hiyo ingebatilisha uchaguzi wa rais Yar´Adua aliyechukua mahamala kwa rais wa zamani Olusegun Obasanjo, taifa hilo lingelazimika kuandaa uchaguzi mwengine, hali iliyohofiwa kwamba ingelitumbukiza taifa hilo kwa machafuko ya kisiasa.


Mzozo huo ulikuwa umeikwamisha serikali ya Rais Yar´Adua katika utekelezaji wa maamuzi muhimu, na kuathiri sekta ya uekezaji nchini humo.


Hii si mara ya kwanza, kwa mahakama kutupilia mbali kesi hiyo, kwani mnamo February mwaka wa 2007, tume iliyobuniwa kuchunguza mamalako kuhusiana na uchaguzi mkuu nchini humo, ilitupilia mbali shinikizo la upinzani kutaka kurejelewa kwa uchaguzi huo.


Rais Yar´Adua mwenyewe alikiri kwamba kulitokea dosari wakati wa uchaguzi huo, lakini akasisitiza kuwa alishinda kwa wingi wa kura na licha ya madai kutoka kwa maafisa wa uchunguzi kwamba uchaguzi huo ulikumbwa na vitisho na udanganyifu kutoka kwa upande wa serikali.


Kufuatia ushindi huo, Rais Yar´Adua hata hivyo bado anakabiliwa na changamoto nyingine za kutimiza ahadi alizotoa wakati wa kampeini za uchaguzi katika kuimarisha sekta ya nishati na usalama katika katika eneo Niger Delta lenye utajiri mkubwa wa mafuta.


Wadadisi wa masuala ya kuichumi wamemlaumu kiongozi huyo kutokana na kujikokota kwa serikali yake kutekeleza mipango ya marekebisho, mbali na kucheleweshwa kwa bajeti ya mwaka ujao na kuteua baraza jipa la mawaziri.


Mnamo mwezi Oktoba mwaka huu Rais Yar´Adua alifanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri hatua iliyosubiriwa kwa hamu na raia wa nchi hiyo ambapo aliwaachisha kazi zaidi ya nusu ya mawaziri wake,lakini akawahifadhi mawaziri wa mafuta na Fedha.Nigeria ni miongoni ma mataifa nanayokumbwa na kiwango cha juu ufasaidi ulimwenguni.


Yar´Adua mwenye umri wa miaka 47, alijitosa siasani siasa na kuwa gavana wa jimbo la Katsina kati ya Mei 1999 hadi May 2007 wakati alipochakuliwa kuliongoza taifa hilo.








Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW