1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi za hatari kwa ustawi wa watoto zaongezeka Ujerumani

2 Agosti 2023

Ofisi ya Ustawi wa vijana Ujerumani imeeleza kuwa takwimu mpya zinaonyesha watoto wengi zaidi nchini humo wapo katika hatari ya kutelekezwa au kupitia unyanyasaji wa kisaikolojia, kimwili au kingono.

Symbolbild | Gewalt gegen Kinder
Picha ya mtoto akifanyiwa kitendo cha ukatili na mtu mzimaPicha: Annette Riedl/dpa/picture alliance

Ofisi za ustawi wa vijana za Ujerumani mwaka jana ziliripoti rekodi ya idadi ya watoto ambao ustawi wao ulikuwa hatarini, na kesi 62,300 zimesajiliwa, kulingana na Ofisi ya Takwimu ya Shirikisho la Ujerumani (Destatis).

Kulingana na Ofisi ya Takwimu ya Shirikisho la Ujerumani (Destatis) mwaka uliopita, ofisi za ustawi wa vijana za Ujerumani ziliripoti rekodi ya idadi ya watoto ambao ustawi wao ulikuwa hatarini, na visa 62,300 zimesajiliwa. Imesema watoto wanne kati ya watano walioathiriwa ni chini ya miaka 14 na karibu nusu chini ya miaka 8.

Soma pia:Mama Mjerumani afungwa kwa kumchuuza mwanawe kwa wabakaji 

Idadi hiyo inawakilisha ongezeko la 4%, au kesi 2,300, ikilinganishwa na 2021. Kwa jumla kesi 203,700 za hatari zinazoshukiwa kwa ustawi wa watoto zilitathminiwa na mamlaka ya ustawi wa vijana. 

Picha ya kivuli cha mtoto, anaekumbana na hali ya ukatiliPicha: Patrick Pleul/dpa/picture alliance

Hatari hizo ni pamoja na zile zinazosababishwa na kupuuzwa, unyanyasaji wa kisaikolojia au unyanyasaji wa kimwili, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kingono.

Mamlaka hiyo imeainisha uwepo wa kupuuzwa kesi zipatazo 59%, huku theluthi moja ya watoto walioathirika wakionesha dalili za kupitia unyanyasaji wa kisaikolojia. Ukatili wa kimwili ulihusika kwa asilimia 27 ya visa vilivyorekodiwa, huku 5% ya watoto walionyesha dalili za kunyanyaswa kingono.

Je takwimu zinasema nini zaidi?

Idadi ya watoto wanaohitaji msaada wa elimu, kulingana na mamlaka, pia iliongezeka kwa 2% hadi kufikia 68,900. Na takribani nusu ya watoto walioathirika walikuwa tayari wanapokea huduma za ustawi wa watoto na vijana wakati tathmini ya hatari ilipofanywa.

Soma pia: Homa kali yawakumba watoto wengi nchini Ujerumani

Ingawa idadi ya kesi za siri zilizorekodiwa karibuni hazikuweza kuthibitishwa, lakini zinashukiwa kuwepo pia. Na idadi ya kesi za papo kwa hapo ambazo awali zilikuwa 1% zimeongezeka hadi 10% wakirekodi visa 33,400 kwa mwaka 2022.

Picha ya mwanafunziPicha: Annette Riedl/dpa/picture alliance

Kuanzia 2017 hadi 2020, mwaka wa kwanza wa janga la virusi vya corona idadi ya kesi ilikua kwa kasi ya 9-10% kwa mwaka, ikishuka kidogo katika mwaka wa pili wa janga hilo 2021, kabla ya kuongezeka tena mnamo 2022.

Takwimu hizo mpya zinatolewa huku umaskini ukionekana kuongezeka nchini Ujerumani, ambapo idadi za kaya zinashindwa kumudu chakula cha mara kwa mara chenye lishe na watu wengi kulazimika kutumia akiba yao ya chakula.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW