1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya Gachagua kusikizwa na Jaji Mkuu Kenya

11 Oktoba 2024

Mahakama Kuu nchini Kenya imepitisha uamuzi Ijumaa kwamba kesi ya kupinga mchakato wa kumuondowa madarakani Naibu wa Rais Rigathi Gachagua, ipelekwe kwa mwanasheria mkuu kwa ajili ya kutowa maelekezo zaidi.

Kenyas Vizepräsident Rigathi Gachagua spricht mit den Medien in Nairobi
Picha: Andrew Kasuku/AP/picture alliance

Jaji Lawrence Mugambi amesema kwa kuzingatia maslahi ya umma kwenye kesi hiyo kunahitajika kuundwa jopo la majaji kulitazama suala la hoja ya kumuondowa madarakani Gachagua.

Maamuzi ya Mahakama Kuu yametolewa baada ya Jumanne wiki hii bunge kupiga kura kuunga mkono kuondolewa madarakani kwa naibu huyo wa rais, kwa tuhuma za kuhusika na ufisadi na uchochezi wa chuki za ukabila.

Baraza la Seneti la Kenya linatarajiwa wiki ijayo kujadili tuhuma hizo na kupiga kura ya kuunga mkono kumuondowa au kumbakisha madarakani bwana Gachagua.