1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Kesi ya Imran Khan kusikilizwa ndani ya majengo ya gereza

28 Novemba 2023

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Pakistan aliyefungwa jela Imran Khan amenyimwa nafasi ya kesi yake kusikilizwa katika mahakama ya wazi kama ilivyoagizwa na Mahakama Kuu.

Pakistan | Waziri Mkuu wa zamani na mwanasiasa mkongwe Imran Khan
Waziri Mkuu wa zamani Pakistan Imran KhanPicha: Akhtar Soomro/REUTERS

Serikali ya Pakistan iliwasilisha ripoti kupinga hatua hiyo ikitaja sababu ya maisha ya kiongozi huyo wa zamani kuwa hatarini.

Wakili wake ameeleza kuwa vikao vya mahakama maalum inayosikiliza kesi dhidi ya Khan kuhusu mashtaka ya kuvujisha siri za serikali, vitaendelea ndani ya majengo ya gereza na vitakuwa wazi kwa vyombo vya habari na kwa umma.

Soma pia:Chama cha Khan chatakiwa kutafuta uongozi mpya

Kesi hiyo itaanza upya siku ya Ijumaa. Mahakama imesema imekuwa ikiendesha vikao vya kesi hiyo gerezani tangu Khan alipofunguliwa mashtaka mwezi uliopita.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW