1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Kesi ya kwanza ya jinai dhidi ya Trump yaanza kusikilizwa

15 Aprili 2024

Kesi ya kwanza ya uhalifu kuwahi kufunguliwa dhidi ya rais wa zamani nchini Marekani imeanza mjini New York na kumfanya mshitakiwa Donald Trump kufika mahakamani kuhudhuria vikao vya kwanza vya kesi hiyo ya kihistoria.

Donald Trump
Donald Trump Picha: Angela Weiss/REUTERS

Jaji Juan Merchan ndio anayeongoza keshi hiyo katika mahakama ya Manhattan ambako Trump aliye na miaka 77 alihudhuria na kuwaambia waandishi habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa kesi hiyo kwamba mashitaka dhidi yake ni  fedheha kwa Marekani.

Trump anakabiliwa na kashfa kughushi rekodi za biashara katika mpango wake wa kuficha madai ya ngono na mwigizaji wa filamu Stormy Daniels ili kuficha uvu-njaji wa sheria za uchaguzi alioushinda mwaka 2016.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW