Kesi ya manusura wa Shakahola yaanza kusikilizwa
15 Juni 2023Watu hao 64 walishtakiwa kwa kosa la kukataa kula na kunywa kwa nia ya kujiua walipokuwa wanapokea matibabu.
Zaidi ya washukiwa 10 wanaozuiliwa ikiwa ni pamoja na mhubiri anayetuhumiwa kuwashawishi mamia ya wafuasi wake kufunga kula na kunywa Paul Mackenzie walikuwa wanashindwa kutembea wenyewe kufika mahakamani baada ya kugoma kula wakiwa rumande kwa zaidi ya wiki moja.
Kesi hiyo inasikilizwa wakati idadi ya miili ya watu iliyofukuliwa kwenye msitu wa Shakahola imefika 318 baada ya miili mingine 15 kufukuliwa hapo jana.
Huku hayo yakijiri mawakili wawili wa mhubiri Mackenzie wamejiondoa kuisimamia kesi yake wakiilaumu serikali kwa kuifanya kazi yao kuwa ngumu kwa kutowapa nafasi ya kuwasiliana na mteja wao na washukiwa wengine waliokamatwa. Kwa sasa Mackenzie na washukiwa wengine wanazuiliwa kwenye gereza la mji wa Malindi.