1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya udhalilishaji watoto kingono kurindima mjini Koeln

Sekione Kitojo
10 Agosti 2020

Uhalifu wa kuwadhalilisha watoto kingono umeongezeka sana barani Ulaya ikiwa pia hapa  nchini Ujerumani Uchunguzi uliofanyika katika nyumba ya Joerg L mwishoni mwa mwaka jana umeleta wimbi la matokeo makubwa la wahalifu.

Polizei Köln, BAO Mitarbeiter*innen
Picha: BAO Berg/Polizei Köln

Katika  uchunguzi huo wa  uhalifu wa udhalilishaji watoto  wadogo  kingono kupitia mtandao  wa  kihalifu, washukiwa 10,000 wamechunguzwa. Leo  inaanza  kesi  dhidi ya  uhalifu  huo  mjini Koeln . 

Picha za ngono  na vidio , ambazo polisi  ilizipata kwa  mtu huyo  Joerg L mwenye umri  wa miaka  43, pamoja na  mazungumzo yake  na  kundi la  siri la watu  waliojipa majina ya  bandia  kama Lila06789 Homer Simpson, au Bullseye, zinaelekeza katika  uchunguzi mpana  wa matumizi ya nguvu dhidi ya watoto  katika  historia ya  jamhuri ya Ujerumani.

Uchunguzi uliofanywa na wachunguzi uligundua kuhusu uhalifu mkubwa dhidi ya watotoPicha: Polizei Köln

Soma pia Udhalilishaji wa watoto Ujerumani watisha

Uchunguzi  huo  ulifanyika  katika  nyumba  ambayo inaonekana  ni  makaazi salama ya familia. Majirani  wakiieleza  kuwa familia  nzuri na  ya  kawaida  kwa  nje,  katika  mji  wa  Bergisch Gladbach, kama  anavyokumbuka  Lisa Wagner polisi  aliyekuwapo siku hiyo  ya  uchunguzi , asubuhi ya  tarehe 21 , Oktoba 2019.

Kiasi ya watoto 50 walipatikana  katika nyumba  hiyo, ikiwa ni  pamoja na  mtoto  wa  miezi mitatu. Orodha ya wahalifu  hao  waliotambulika imefikia  watu 87, anasema  Markus Hartmann katika  ofisi  ya waendesha  mashitaka mjini  Koeln, ambaye  anaongoza  kitengo  cha uhalifu wa  mitandaoni.

Wachunguzi wakifanyakazi zao za uchunguzi mjini KoelnPicha: Polizei Köln

Udhalilishaji kingono

Kwa kila  mmoja  katika  watu  hao 87 kuna  ushahidi  mwingine unaopatikana, ambao ni  watu  wengine  wanaofanya  uhalifu  huo. Mwendesha  mashitaka  Hartmann  amesisitiza kwamba:

"Hatukuwa tunajishughulisha  na  mtu mmoja tu, badala yake  wahalifu walikuwa  na  mawasiliano  mazuri, ambayo yaliwezesha  wao  kufanya uhalifu  huo, na kufanikiwa  kuuficha."

Soma pia Udhalilishaji watoto bado tatizo duniani

Uwezekano huu  wa mawasiliano  ndio ulikuwa msingi  mkubwa wa udhalilishaji  huu  kingono. Mwishoni  mwa  mwezi Juni waziri wa  sheria wa  jimbo  la  North Rhine Westfalia  Peter Biesenbach, kwamba wachunguzi wamepata  majina  na  waliko  zaidi ya wahalifu 30,000. Biesenbach  anazungumzia  kuhusu kiwango cha  uhalifu  huo, unaokera. Wachunguzi  wanazungumzia  kuhusu  makundi ya mawasiliano , ambapo kuna watu  zaidi ya  1,800 wanaofanya mawasiliano, kama  anavyoeleza  Markus Hartmann.

Mshitakiwa Bastian S, akisubiri kuanza kwa kesi yake ya udhalilishaji kingono katika jimbo la North Rhine WestfaliaPicha: picture-alliance/dpa/R. Weihrauch

"Ukiangalia kwa kina kuhusu mawasiliano  hayo, utaona kwamba washiriki wa mazungumzo  hayo wanatambua  kuwa  uhalifu dhidi  ya watoto ni  suala  lisilokubalika katika  jamii."

Soma pia Mapadri wahusishwa na udhalilishaji kingono Marekani

Utambuzi kwamba, kuna adhabu  kali kwa watu  wanaofanya  uhalifu huo, ulionekana  katika  mawasiliano  yao  wakionekana kama watu wa kawaida katika  jamii. Lakini  hata  hivyo  watu hao kila mara waliendelea  na  uhalifu  huo.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW