1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya uhaini dhid ya Besigye yaahirishwa, Uganda

24 Februari 2026

Mahakama kuu nchini Uganda imeahirisha kuendeshwa kwa kesi ya uhaini dhidi ya mwanasiasa wa upinzani Dokta Kizza Besigye. Hii ni baada ya upande wa mashtaka kusema unahitaji muda wa wiki moja zaidi kupanga ushahidi.

Uganda 2026 | Oppositionsführer Dr. Kizza Besigye wegen Hochverrats vor Gericht
Kesi ya uhaini dhid ya Besigye yaahirishwa, UgandaPicha: Lubega Emmanuel/DW

Mawakili wa washtakiwa wakiongozwa na Martha Karua kutoka Kenya wamemuomba jaji kuwawajibisha waendesha mashtaka kwa upande wa serikali kwa kutotimiza agizo la kutokabidhi ushahidi wote wanaolenga kuwasilsha katika kusikilizwa kwa kesi hiyo ya uhaini.

Mwezi Desembamwaka jana walipewa hadi tarehe 21 Januarimwaka huu kukabidhi ushahidi huo lakini wiki iliyopita waliweza wakutoa jalada moja tu la kurasa zaidi ya 2000 wakisema kuwa wanaandaa zingine mbili zikiandamana na kanda za video pamoja na sauti za simu kama miongoni mwa ushahidi wao.

Mawakili Martha Karua pamoja na Shariff Wafula wameimbia hivi DW  kuhusu kero yao juu ya  mwenendo wa upande wa mashtaka kudoroza kesi hiyo.

Mawakili wa washtakiwa wamemuomba jaji kuwawajibisha waendesha mashtaka kwa upande wa serikali kwa kutotimiza agizo la kutokabidhi ushahidi wote wanaolenga kuwasilsha katika kesi dhidi ya Dr. Kizza Besigye na wenzakePicha: Lubega Emmanuel/DW

"Hakuna kitu kinaendelea kwa sababu hatujaanza kesi rasmi upande wa mashtaka ukisema hawako tayari” "Yaani hayo yote ni michezo ya upande wa mashtaka kwa ajili tangu mwaka jana 2025 walikuwa wakielezea kuwa wana ushahidi kamilifu watakaowasilisha”

Kuburuzwa  kesi hiyo hasa baada ya mahakama kutupilia mbali ombi la washtakiwa Dokta Kizza Besigye, Obed Lutale pamoja mwanajeshi Kapteni Dennis Oola mara nyingi kumefasiliwa kuegemea hila za kisiasa za utawala wa rais Museveni ambaye hapo jana aliagiza kutofanyika kwa maombi maalum kwa ajili ya Dokta Besigye na wafungwa wengine wa kisiasa.

Museveni akataa maombo maalum kufanyika kwa Besigye 

MKe wa Besigye Mhandisi Winnie Byanyima ambaye alikuwa ameandaa kufanyika kwa maombi hayo katika kanisa kuu la kikatoliki la Rubaga jijini Kampala amemwondolea lawama askofu mkuu Paul Semwogerere kwa kuahirisha maombi hayo. Hii ni baada ya umma kutoa shtuma na ukosoaji dhidi ya askofu huyo kiongozi wa waumini wa kikatoliki Uganda.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni Picha: AFP

"Najivunia askofu wetu mkuu Paul Semwogerere ambaye alimpinga rais Museveni alipomwagiza kutoendesha maombi hayo lakini akamjibu kuwa hii italeta chuki zaidi dhidi yake rais mwenyewe wakakubaliana waahirishe,Jenerali Museveni na wamawawe wanadhani kuwa watadhibiti maisha yetu hata ya kiroho”

Jaji Emmanuel Baguma ametenga tarehe 12 mwezi ujao wa Machi kuwa siku ya kuanza kupanga kusikilizwa kwa kesi hiyo. Awali wakili Martha Karua alilalamikia jinsi alivyovunjiwa heshima na hadhi yake na askari polisi mwanamke alipokuwa akiingia mahakamani kwa matamshi kuwa kesi hiyo haihusu taifa la Kenya.

Itakumbukwa kuwa Dokta Besigye alikamatwa Kenya akiwa na mwenzake Obed Lutale na walifikishwa Uganda katika hali ambayo ilielezewa walitekwa kinyume na sheria za Kenya.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW