1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya uhalifu wa kivita Darfur yaanza kusikilizwa ICC

21 Mei 2021

Shirika la Human Rights Watch limesema kesi ya kwanza katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC dhidi ya Ali Kosheib ni hatua muhimu katika upatikanaji haki kwa uhalifu wa Darfur, Sudan. 

Südafrika Omar al-Baschir in Johannesburg
Picha: Reuters/S. Sibeko

Shirika hilo linalofuatilia haki za binadamu limesema hata hivyo, kutofikishwa kwa washukiwa wengine wanne katika mahakama hiyo akiwemo rais wa zamani wa Sudan, Omar al Bashir kunatoa umuhimu wa serikali ya Sudan kuwafikisha kwa haraka bila kuchelewa katika mahakama ya ICC 

Ali Kosheib alikuwa kiongozi wa kundi la wanamgambo la ''anjaweed'' aliyeshikilia pia nafasi ya ukamanda katika jeshi la ulinzi la Sudan.

Aprili 27 mwaka 2007 mahakama ya ICC ilitoa waranti ya kwanza ya kukamatwa kwa Kosheib, baada ya kumshitaki kwa makosa 50 ya uhalifu dhidi ya binaadamu na uhalifu wa kivita kwa shutuma za ubakaji, uharibifu wa mali na kuuwawa kwa wakaazi wa vijiji vinne magharibi mwa Darfur mwaka 2003 na 2004.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW