1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khamenei aagiza kuendelea kufungwa kwa Mlango Bahari, Hormuz

12 Machi 2026

Kiongozi mkuu mpya wa Iran Ayatollah Mojtaba Khamenei, ameagiza njia muhimu ya safari za meli za mafuta ya Mlango-Bahari wa Hormuz iendelee kufungwa.

Iran Tehran 2024 | Mojtaba Khamenei
Kiongozi mkuu mpya wa Iran Ayatollah Mojtaba KhameneiPicha: khamenei.ir/AFP

Khamenei, ambaye inadaiwa alijeruhiwa katika shambulizi la anga, bado hajaonekana hadharani tangu kuteuliwa kwake Jumapili iliyopita kama kiongozi mkuu, na ujumbe wake ulisomwa kupitia televisheni ya kitaifa.

Khamenei pia ametaka mataifa ya ghuba kufunga kambi za kijeshi za Marekani.

Ameongeza kuwa kiasi kidogo cha kisasi cha Iran kwa mashambulizi ya Marekani na Israel kimechukuwa mweleko thabiti lakini kwamba hadi kitakapotekelezwa kikamilifu, suala hilo litasalia kuwa miongoni mwa vipaumbele vyao.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW