1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Khan aitisha maandamano ya nchi nzima Pakistan

14 Mei 2023

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan, ametoa wito wa maandamano ya uhuru nchini kote leo, baada ya kukamatwa kwake katika kipindi kifupi na kuwekwa kizuizini hatua iliyosababisha machafuko mabaya.

Pakistan Ex-Premierminister Imran Khan
Picha: Imran Khan/Twitter/REUTERS

Katika hotuba yake aliyoitoa kupitia mtandao wa YouTube, Khan amesema "Uhuru hauji kirahisi. Lazima upokwe kwa nguvu. Unapaswa kujitoa kwa ajili uhuru huo."Aidha ametoa wito kwa wafuwasi wake kushiriki maandamano katika maeneo ya vijiji na mitaa yao jioni ya leo kujitokeza kwa saa moja nchini kote kuanzia saa 11:30.Baada ya siku tano za ghasia kote Pakistan, asubuhi ya leo Jumapili ilikuwa na utulivu, lakini Khan ameahidi kurejea kufanya kampeni siku ya Jumatano kwa ajili ya uchaguzi ulioitishwa mapema wa taifa hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW