KHARTOUM: Bashir akana serikali yake haikuhusika na ukiukaji wa haki za binadamu
20 Machi 2007Matangazo
Rais wa Sudan, Omar el Bashir, amekanusha madai kwamba serikali yake imehusika katika vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu katika jimbo la Darfur.
Akizungumza kuhusu hali ya Darfur katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema hali ni ya kuvunja moyo.
´Ninajua kwamba kuna hali ya kuvunjika moyo inayozidi miongoni mwa wanachama wa Umoja wa Mataifa hususan katika baraza la usalama. Hata sisi tumevunjika moyo, lakini la muhimu ni kwamba mchakato wa kisiasa bado unaendelea.´
Inakadiriwa watu laki mbili wameuwawa na wengine zaidi ya milioni 2.5 kulazimika kuyakimbia makazi yao tangu mzozo wa Darfur ulipozuka. Marekani imeyaeleza mauaji ya watu hao kuwa ya halaiki.