1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Hayati John Garang aombolezwa

5 Agosti 2005

Raia wa Sudan kwa maelfu,wametoa heshima ya mwisho kwa makamu wa rais na kiongozi wa zamani wa waasi John Garang,aliefariki katika ajali ya ndege ya helikopta.Garang atazikwa Juba,mji mkuu wa eneo la kusini la Sudan lenye utawala wa ndani.Inatazamiwa kuwa hadi waombolezaji nusu milioni watahudhuria maziko yake.Kifo cha Garang kilizusha machafuko ya siku 3 kati ya Wasudani wa kaskazini na wa kusini.Si chini ya watu 130 wamepoteza maisha yao na kiasi ya 359 wengine wamejeruhiwa katika mapambano hayo.Garang, alikiongoza chama cha Ukombozi wa Watu wa Sudan katika mapambano makali ya miaka 21,dhidi ya serikali inayodhibitiwa na Waarabu,kabla ya kutia saini makubaliano ya amani mwezi wa Januari.Kifo chake kimetokea hata kabla ya kutimiza mwezi mmoja tangu kuwa makamu wa kwanza wa rais kuambatana na makubaliano ya amani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW