1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khartoum. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa ziarani nchini Sudan, katika jimbo lililokumbwa na machafuko la Dafur.

29 Mei 2005

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bwana Kofi Annan ametembelea jimbo lililo na machafuko la Dafur kama sehemu ya ziara yake ya siku tatu nchini Sudan. Baada ya mazungumzo na serikali ya Sudan , Annan alitembelea moja kati ya makambi makubwa nchini humo kwa ajili ya watu walioyakimbia makaazi yao, ambalo lina watu kiasi cha 110,000.

Bwana Annan aliwaambia waandishi wa habari kuwa eneo la kusini lililokumbwa na vita halipaswi kutelekezwa.

Umoja wa mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu 180,000 wameuwawa na kiasi cha watu milioni mbili wamelazimika kuyakimbia makaazi yao kutokana na vita vya waasi na mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya vijiji yanayofanywa na wale wanaojulikana kama wanamgambo wa Janjaweed.

Wachunguzi wa mambo wanasema kuwa serikali ya Sudan inawaunga mkono Janjaweek.

Wafadhili katika mkutano wao nchini Ethiopia wameahidi mamia ya mamilioni ya Euro kulisaidia jeshi la kulinda amani la umoja wa Afrika katika jimbo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW