1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khartoum. Marekani yaondoa baadhi ya vikwazo.

13 Novemba 2005

Marekani imekubali kuondoa baadhi ya vikwazo vya kiuchumi ilivyoiwekea Sudan , na kuondoa hatua ya marufuku dhidi ya upelekaji wa treni zilizotengenezwa nchini Marekani ili kusaidia utekelezaji wa makubaliano ya amani kati ya upande wa kusini na kaskazini nchini humo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Sudan Lam Akol Ajawin amesema suala la vikwazo ni moja kati ya masuala muhimu yaliyojadiliwa katika ziara mjini Washington mapema mwezi huu iliyofanywa na makamu wa rais na kiongozi wa chama kutoka kusini mwa nchi hiyo Salva Kiir.

Amewaambia waandishi wa habari kuwa licha ya kuwekwa tena vikwazo, lakini ujumbe huo umefanikiwa katika kuwashawishi maafisa wa Marekani kuondoa marufuku dhidi ya kupelekwa nchini Sudan kwa treni zilizotengenezwa nchini Marekani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW