1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM. Mchunguzi maalum wa umoja wa mataifa kupelekwa Darfur.

22 Aprili 2005

Tume ya umoja wa mataifa ya haki za binadamu imeafiki kumchagua muwakilishi maalum atakae chunguza jinsi haki za binadamu zinavyo shughulikiwa katika jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan.

Mchunguzi huyo maalum atahitajika kutoa taarifa kwa tume ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa na vile vile kwa baraza kuu la umoja wa mataifa.

Azimo hili linafuatia makubaliano katika mkutano uliofanyika Geneva kati ya maataifa ya Ulaya na Afrika, ambako mataifa haya yanavilaani vitendo vya maujaji katika jimbo la Darfur lakini bila kuishurutisha serikali ya Khartoum kama Umoja wa nchi za Ulaya ulivyotaka.

Zaidi ya watu 180,000 wameuwawa na wengine zaidi ya watu milioni mbili wamelazimika kuyahama makaazi yao kukimbia vita vilivyozuka miaka miwili iliyopita katika jimbo la Darfur.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW