KHARTOUM: Rais Bashir alipongeza kundi la SPLM
11 Agosti 2005Matangazo
Rais Omar el- Bashir wa Sudan amelipongeza kundi la SPLM nchini humo kwa kuonyesha ushujaa baada ya kifo cha John Garang. Katika sherehe ya kuapishwa Silva Kiir, kuwa makamu wa rais wa Sudan, rais Bashir amesema leo ni siku ya huzuni na furaha kwa Sudan.
Kiir ameichukua nafasi iliyowachwa na marehemu John Garang, aliyefariki dunia katika ajali ya helikopta majuma mawili yaliyopita. Ameapa kuuendeleza mpango wa amani uliosainiwa mwezi Januari mwaka huu unaolenga kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya eneo la kazkazini na kusini, ambavyo vilisababisha vifo vya watu milioni mbili. Kiir ameahidi pia kufuata nyayo za Garang na kuimarisha umoja wa taifa.