1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Rais Kagame wa Rwanda ziarani Sudan

23 Februari 2005

Rais wa Rwanda Paul Kagame yupo nchini Sudan kwa ziara ya siku tatu ambapo atatembelea eneo la mzozo la Darfur.Kagame amefanya mazungumzo na mwenyeji wake rais wa Sudan Omar Al- Bashir na kuzungumzia masuala yanayohusu nchi hiyo pamoja na masuala ya kimataifa pamoja na mzozo wa Darfur.

Takriban wanajeshi 400 wapo katika eneo la Darfur katika mpango wa kukomesha mapigano wa Umoja wa Afrika.

Rais Kagame amepangiwa pia kukutana na baadhi ya maafisa wakuu mjini Khartoum na kisha kuelekea katika eneo la El- Fashir ambako kuna makao ya Ujumbe wa Umoja wa Afrika.Maelfu ya watu walipoteza maisha yao katika kipindi cha miaka miwili ya vita kati ya majeshi ya serikali ya Khartoum na makundi mawili ya waasi katika eneo la Darfur na zaidi ya milioni wayahama maskani yao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW