1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khartoum. Sudan yapuuzia vitisho vya marufuku ya kurusha ndege Darfur.

15 Desemba 2006

Serikali ya Sudan imepuuzia vitisho vya serikali ya Uingereza vya kuweka marufuku ya kutorushwa ndege katika eneo la Darfur iwapo serikali ya Sudan itaendelea kupinga kuwekwa kwa majeshi ya umoja wa mataifa ya kulinda amani. Blair ametoa uwezekano huo wa marufuku ya kurusha ndege wakati wa mkutano wiki iliyopita na rais George W. Bush. Hatua hiyo italenga katika kusitisha matumizi ya ndege za kijeshi za serikali ya Sudan zinazosaidia mashambulizi dhidi ya vijiji katika jimbo la Darfur. Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni nchini Sudan amesema kuwa Khartoum inaikaribisha ziara ya ujumbe wa baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa iwapo itaangalia ukweli unaotokea katika jimbo hilo.