1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM : Umoja wa Afrika washutumu serikali ya Sudan kwa kushambulia raia huko Dafur

2 Oktoba 2005

Umoja wa Afrika umevishutumu vikosi vya serikali ya Sudan kwa kuwashambulia raia huko Dafur,kufanya uharibifu wa kukusudia na wa kikware ambao umepelekea kuuwawa kwa watu 44 na kuwapotezea makaazi wengine maelfu katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Mwakilishi mkuu wa Umoja wa Afrika kwa Sudan Balozi Baba Gana Kingibe akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Khartoum ametaja matukio manne ya jeshi la Sudan kufanya kile alichookita mashambulizi yaliyoratibiwa kwa pamoja na wanamgambo wa Kiarabu wa kundi la Janjaweed tokea tarehe 18 mwezi wa Septemba huko Dafur.

Madai yake ni karaha ya kisiasa kwa serikali mpya ya Sudan ambayo imekuwa ikikanusha mara kwa mara kuwepo kwa ushirikiano wowote ule na Janjaweed ambayo inalaumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu katika mzozo huo wa miaka miwili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW