1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Wasudani waafikiana kugawana mali

22 Desemba 2003

Wajumbe wa serikali ya Sudan na chama kikuu cha waasi wa kusini mwa nchi hiyo katika majadiliano ya amani wameafikiana jinsi ya kugawana mapato ya utajiri wa mafuta ya petroli huku wakiahidi kurefusha sherehe rasmi za kutia saini mkataba kamili hadi baadaye mwakani. Msimamizi wa majadiliano hayo ambayo ni Jenerali mstaafu wa Kenya, Lazarus SUMBEIYO, amekataa kueleza zaidi kuhusu viwango vya mapato ya mafuta vilivyokubaliwa kutolewa kwa kila upande. Waziri wa mambo ya nje wa Kenya, Kalonzo MUSYOKO amesema kwa upande wake kuwa mkataba kamili umeahirishwa hadi katikati mwakani ili kutoa nafasi zaidi kwa serikali ya Khartoum na wapiganaji wa SPLA kukamilisha hatua za utekelezaji wa mapatano hayo. Watu milioni 2 wanasadikiwa wamekufa katika miaka 20 ya vita vya kiraia vinavyoendelea nchini Sudan.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW