Khartoum:Benki ya dunia yakataa kutoa fedha.
11 Agosti 2006Serikali ya kusini mwa Sudan imeshindwa kufuata masharti magumu ya Benki kuu ya Dunia juu ya hatua ya mikataba ya kandarasi ya ujenzi wa miundo mbinu.
Kiongozi wa zamani wa waasi ambae anaeongoza huko kusini amekata tamaa juu ya kuujenga upya mji huo wenye ukosefu wa maji, umeme na njia za kuaminika baada ya zaidi ya miaka 20 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Benki ya dunia inayomiliki mfuko wa maendeleo ya jamii wenye kutoa mamilioni ya dollar imesema, serikali ya kusini mwa Sudan imetumia vibaya fedha za ujenzi wa mji mkuu wao wa Juba.
Wakaazi wengi wa kusini mwa Sudan wanalalamika kuwa hawajapata manufaa yoyote ya makubaliano ya amani na Khartoum yaliyotiwa saini mwaka jana, wakiwaweka viongozi wao katika wakati mgumu katika kuharakisha hudum,a za kijamii zikiwemo za kimatibabu, shule na bara bara.