1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM:Hali nchini Sudan

4 Agosti 2005

Takriban watu 130 wameuwawa na wengine 350 wakajeruhiwa nchini Sudan baada ya siku tatu za ghasia kufuatia kifo cha kiongozi wa waasi na makamu wa kwanza war ais nchini humo John Garang.

Wakaazi wa sudan wamearifu imekuwa hatari kutembea mjini Khartoum hasa nyakati za usiku kinyume ilivyokuwa awali.

Ghasia pia zimeripotiwa katika miji ya Makalal ambapo watu 6 wameuwawa na Juba kutakakofanyika maziko ya Garang watu 13 wameuwawa.

Ubalozi wa Marekani mjini Khartoum umewaonya raia wake kutotembea mjini Khartoum kufuatia hali ya usalama.wakati huo huo pia wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imewaonya raia wake kutosafiri Sudan hadi hali itakapoimarika.

Taarifa nyingine zimearifu serikali ya Uganda imeitisha mkutano wa dharura baina ya viongozi wa Afrika Mashariki kujadili hali ya Sudan.Serikali hiyo pia imelazimika kuhairisha maombolezi ya kitaifa hii leo ya watu wanane waliouwawa katika ajali ya ndege pamoja na makamu wa rais wa kwanza wa Sudan John Garang.

Serikali ya Sidan imekataa kuzitoa maiti hizo hadi uchunguzi wa ajali ya ndege hiyo utakapokamilika

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW