1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM:Je rais Omar al Bashir ataongeza muda wa kikosi cha AU huko Darfur

19 Septemba 2006

Serikali ya Sudan inatarajiwa kukubali kuongeza muda wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika katika jimbo la mgogoro la Darfur wakati wa mkutano wa viongozi wa Afrika mjini NewYork wiki hii.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir anahinikizwa kuruhusu wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa katika jimbo la Darfur wakati muda wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika utakapomalizika Septemba 30.

Kikosi cha wanajeshi 7,000 wa Umoja wa Afrika kimeshindwa kumaliza mgogoro katika jimbo hilo ambapo watu kiasi cha laki mbili wameuwawa na kusababisha maafa makubwa ya kibinadamu duniani.

Umoja wa mataifa unataka kuchukua nafasi ya kulinda amani kwenye jimbo hilo ukiwa na kikosi cha wanajeshi 20 elfu,Lakini rais wa Sudan Omar al- bashir anashikilia hadi sasa kwamba hawezi kuruhusu wanajeshi hao kuingia Darfur.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW