1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM.Mapigano mapya yazuka Sudan

22 Juni 2005

Mapigano mapya yamezuka kaskazini mashariki mwa Sudan baina ya vikosi vya serikali na waasi ambao wanataka kuudhibiti mji wa Tokar ulio kilomita 120 kutoka bandari ya Sudan.

Kundi la waasi la Beja Congress linadai kunyanyaswa na serikali huku utawala wa Sudan ukilaumu machafuko hayo yanachochewa na waasi kutoka jimbo la magharibi la Darfur.

Vile vile serikali ya Sudan inawalaumu jirani zake Eritrea kwa kuwaunga mkono waasi wa kundi la Beja katika mapigano hayo.

Mapigano hayo yanarudisha nyuma juhudi za kutafuta amani wakati ambapo mwishoni mwa wiki serikali ya Sudan ilitia saini mkataba wa maelewano na kundi kubwa la waasi la National Democratic Alliance.

Mazungumzo yanaendelea mjini Abuja Nigeria ili kutafuta mbinu za kumaliza ukaidi wa vikundi vya waasi wa magharibi mwa Sudan ambako zaidi ya watu laki moja na elfu themanini wameuwawa na wengine milioni mbili kuyahama makaazi yao kwa sababu ya vita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW