1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM.Mwakilishi wa umoja wa mataifa atii amri na kuondoka Sudan

24 Oktoba 2006

Mwakilishi wa umoja wa mataifa nchini Sudan Jan Pronk ameondoka kutoka nchini humo baada ya utawala wa Sudan kumtaka afanye hivyo.

Pronk aliamriwa kuondoka kutoka nchini Sudan baada ya kuandika katika mtandao wake wa kibinafsi kuwa jeshi la Sudan linakabiliwa na hali ya kuvunjika moyo na pia limeshindwa vibaya katika vita dhidi ya waasi wa jimbo la Darfur magharibi mwa nchi hiyo.

Jan Pronk ambae amewasili mjini New York anatarajiwa kushauriana na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffi Annan, msemaji wa umoja wa mataifa amedokeza kuwa katibu mkuu Koffi Annan ana imani kubwa na bwana Pronk.

Sudan imekuwa ikipinga hatua ya kupelekwa nchini humo wanajeshi 20,000 wa kulinda amani wa umoja wa mataifa kuchukuwa mahala pa kikosi cha wanajeshi 7,000 wa umoja wa nchi za Afrika AU.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW