KHARTOUM:Sudan yakubali majeshi ya UNO na AU
18 Juni 2007Matangazo
Serikali ya Sudan imekubali bila ya masharti yoyote kuyaruhusu majeshi ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika yalinde amani katika jimbo la Darfur.Habari hizo zimethibitishwa na serikali hiyo pamoja na ujumbe wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa uliofanya mazungumzo na rais Omar Bashir wa Sudan.
Jeshi hilo litakuwa na askari alfu 19.