KHARTOUM:Sudan yakubali wanajeshi wa Au na Um
13 Juni 2007Serikali ya Sudan imekubali mapendekezo ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika ya kutuma vikosi vyake katika eneo la mgogoro la Darfur.
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu hatimaye pande hizo tatu zimeafikiana kutumwa kwa jeshi la mseto litakalojumuisha wanajeshi 20 elfu kutika Umoja wa Afrika na Umoja wa mataifa pamoja na maafisa wa polisi ambao wengi watatoka Afrika.
Akitangaza maafikiano hayo mbele ya waandishi wa habari Balozi Said Geenit alisema.
Hata hivyo Marekani inashuku ikiwa kweli serikali ya mjini Khartoum itakuwa muanifu katika mpango huo.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Sean MacCormack amesema rais Omar al Beshir ameshindwa kutimiza ahadi zingine katika miaka ya nyuma. Mgogoro wa Darfur ulianza mwaka 2003 na kusababisha kiasi cha watu laki mbili wameuwawa na wengine zaidi ya millioni mbili kulazimika kuhama makaazi yao.