1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kibarua cha kocha wa timu ya taifa ya Mali chaota nyasi

14 Juni 2024

Mali imemfuta kazi kocha mkuu Eric Chelle. Haya ni kwa mujibu wa shirikisho la soka la taifa hilo la Afrika Magharibi.

Mali
Wafuasi wa timu ya kitaifa ya Mali Picha: AFP via Getty Images

Katika taarifa iliyopeperushwa kutipia televisheni ya taifa, shirikisho hilo halikutoa sababu ya uamuzi wa huo lakini hatua hii inajiri siku chache baada ya Mali kulazimishwa sare ya bila kufungana na wachezaji 10 wa Madagascar katika mechi ya Kundi I ya kufuzu kwa Kombe la Dunia mjini Johannesburg.

Chelle, mwenye umri wa 46, mzaliwa wa Ivory Coast kwa baba Mfaransa na mama kutoka Mali, alilelewa Ufaransa. Alicheza katika ngazi ya klabu nyingi nchini Ufaransa na Mali katika ngazi ya kimataifa.

Aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa Mali mnamo Mei 2022 na kuiongoza timu hiyo kutinga robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika la 2023 lililofanyika Ivory Coast mapema mwaka huu.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW