Kiev. Bunge lamuidhinisha Yanukovich.
5 Agosti 2006Matangazo
Bunge la Ukraine limemthibitisha mwanasiasa ambaye anaegemea upande wa Urusi Viktor Yanukovich kuwa waziri mkuu, na kumaliza mzozo wa kisiasa uliodumu kwa miezi minne.
Wabunge wamemuidhinisha Yanukovich kwa kura 271 dhidi ya 9, huku wengi wa wabunge wanaopendelea nchi za magharibi wakisusia kupiga kura ama kutohudhuria kikao hicho.
Kura hiyo ilifanyika siku moja baada ya rais anayeegemea upande wa mataifa ya magharibi Viktor Yushchenko kumuunga mkono hasimu wake katika mapinduzi yanayojulikana kama ya rangi ya chungwa. Yushchenko amesema kuwa pendekezo la kuvunja bunge la kuitisha uchaguzi upya lingekuwa ni pigo kwa nchi hiyo.