1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV: Putin aitembelea Ukraine

19 Machi 2005

Rais Vladimir Putin wa Russia hii leo anaizuru Ukraine.Hii ni ziara yake ya mwanzo nchini Ukraine tangu serikali mpya kushika madaraka chini ya uongozi wa Viktor Yushchenko anaelemea upande wa magharibi kisiasa.Ziara hii inatazamwa kama ni ishara ya kuafikiana,baada ya Putin hapo awali kumuunga mkono hadhrani Viktor Yanukowitsch aliekuwa mpinzani mkuu wa Jushchenko wakati wa uchaguzi.Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya kigeni mjini Moscow,majadiliano hasa yatakuwa juu ya uhusiano wa siku zijazo kati ya nchi hizo mbili. Jushchenko amesema angependa kuwa na uhusiano mzuri pamoja na Moscow,lakini lengo muhimu kabisa la kisiasa ni kuijumuisha Ukraine na Umoja wa Ulaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW