Kiev yashambuliwa tena kwa droni za Urusi
4 Julai 2025
Mkuu wa jeshi kwenye mji huo, Tymur Tkachenko, ameandika kupitia chaneli ya Telegram kwamba maeneo kadhaa ya wilaya ya Solomianskyi yanawaka moto kutokana na mashambulizi hayo.
Tkachenko amesema kuna uwezekano wa watu kuuawa na kujeruhiwa kwa sababu sehemu zinazowaka moto ni makaazi ya raia, ingawa hakuthibitisha idadi rasmi.
Madhara ya droni hizo yameripotiwa pia kwenye maeneo mengine manne ya mji mkuu, Kiev.
Jeshi la anga la Ukraine limesema Urusi imerusha pia kombora moja la mwendo wa kasi.
Mapema, gavana wa mkoa wa Donestk aliripoti kwamba watu watano waliuawa na wengine 12 kujeruhiwa kutokana na mashambulizi ya Urusi katika mkoa wake.
Ukraine imekuwa ikisaidiwa na mataifa ya Magharibi kukabiliana na uvamizi wa Urusi kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.