SiasaUkraine
Mji wa Kiev washambuliwa tena na Urusi
1 Juni 2023Matangazo
Watu wengine 14 wameripotiwa kujeruhiwa katika mashambulizi hayo, ambayo ni ya 18 kuulenga mji mkuu huo wa Ukraine mnamo mwezi Mei.
Meya wa Kiev Vitali Klitschko amesema jengo la makaazi ya watu pamoja na kituo cha afya vimeharibiwa. Wakati huo huo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amearifu kuwa amekwenda nchini Moldova kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya, ambako anatarajiwa kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana na viongozi kadhaa wa mataifa ya Ulaya.
Katika mazungumzo hayo, amesema ataomba msaada wa ndege za kivita zitakazoisaidia nchi yake kukabliana na mashambulizi ya Urusi.