1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV: Yushchenko aitimua serikali nzima

9 Septemba 2005

Rais Viktor Yushchenko wa Ukraine ameifukuza serikali ya waziri mkuu Yulia Tymoshenko,miezi tisa tu baada ya wanasiasa hao wawili kuongoza kile kilichokuja kujulikana kama “orange revolution”.Serikali hiyo imefukzwa baada ya maafisa fulani wa ngazi ya juu kujiuzulu kwa sababu ya suala la rushwa.Yushchenko amemteua mtaalamu wa kiuchumi Yuri Yekhanurov,mwenye asili ya Kirussia kushika wadhifa wa waziri mkuu kwa muda.Kashfa ya rushwa ilianza jumamosi iliyopita,mkuu wa majeshi alipojiuzulu akisema rais amezungukwa na watu wanaopokea hongo.Yushchenko alichaguliwa Desemba mwaka jana katika uchaguzi wa rais uliyoitishwa upya.Maandamano makubwa yaliofanywa baada ya uchaguzi wa mwanzo,yalikuja kuitwa “orange revolution”.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW