1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiev.Hali ya wasi wasi yazidi.

5 Aprili 2007

Rais wa Ukraine Viktor Yushchenko ameongeza hali ya wasi wasi katika mvutano na waziri wake mkuu.

Ametoa onyo kwa wabunge kuwa wakikaidi amri yake ya kufanya uchaguzi mpya wa bunge , watakabiliwa na mashtaka ya uhalifu.

Waziri mkuu Viktor Yanukovich na utawala wake wa serikali ya muungano bungeni amekataa kukubali amri hiyo ya rais, wakisema kuwa watasubiri hadi pale mahakama ya katiba itakapotoa uamuzi wake.

Mzozo huo kati ya rais Yushchenko anayeunga mkono mataifa ya magharibi na waziri mkuu Yanukovich anayeunga mkono Russia umesababisha maelfu ya waandamanaji kuingia mitaani mjini Kiev wakipinga amri hiyo ya rais.