KIEV:Mzozo wa Ukraine waendelea
9 Septemba 2005Matangazo
Rais Vicktor Yushenko amewataka wabunge wamuunge mkono waziri mkuu mteule Yury Yekhanurov.
Yury Yekhanurov anahitajika kuidhinishwa na bunge ambako wanamuunga mkono rais Yushenko hawana wingi.
Yekhanurov ameteuliwa baada ya kutimuliwa kazini waziri mkuu Yulia Tymoshenko na baraza lake hapo jana kwa madai ya kuhusika na vitendo vya rushwa.
Mzozo wa Ukraine umefuatia hali mvutano kati ya rais Yushenko na waziri mkuu Tymoshenko juu ya mwelekeo wa kiuchumi nchini humo.