1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiChina

Kufilisiwa kwa Evergrande na athari zake kwa China

30 Januari 2024

Mahakama ya Hong Kong imeiamuru kampuni kubwa ya ujenzi wa nyumba ya China kuingia katika muflisi. Kufungwa kwa kampuni hiyo kunaweza kuathari uchumi wa China inayoshika nafasi ya pili ya nguvu ya uchumi duniani.

Hong-Kong | Mahakama Kuu
Mahakama Kuu Hong Kong ambako kesi dhidi ya kampuni ya Evergrande ilitolewa hukumu.Picha: Vernon Yuen/picture alliance /AP

Kampuni hiyo Evagrande imesema kuwa itaendelea na shughuli zake licha ya hukumu  ya mahakama. 

Mashtaka dhidi ya kampuni ya Evergrande yaliwasilishwa na kampuni ya uekezaji ya Top Shine iliyosajiliwa na Samoa, moja ya kampuni tanzu za Evergrande, miongoni mwa zingine.

Jaji wa Mahakama Kuu Linda Chan amesema kampuni  ya  Evergrande haikuonesha wazi hatua za marekebisho na  kwamba hukumu ya kuifunga kampuni hiyo imestahili.

Soma pia:China yaongeza shinikizo la kijeshi kwa Taiwan baada ya ziara ya maafisa wa marekani

Msako ambao umekuwa unafanywa na China miaka mitatu  iliyopita dhidi ya ulanguzi wa miaka zaidi ya 20 katika sekta  binafsi ya ujenzi, ulitifua mgogoro mkubwa na kusababisha  deni la dola bilioni 300 kwa kampuni hiyo ya ujenzi wa nyumba.

Miezi michache baadaye kampuni hiyo ilishindwa kulipa madeni yake na pendekezo lake juu ya kubadilisha utaratibu  wa malipo ya deni hilo lilikataliwa na wadai.

Mchakato wa kutekeleza hukumu hiyo

Hukumu iliyotolewa na mahakama itasababisha mchakato wa muda mrefu wa kuzifilisi mali za kampuni ya Evergrande  pamoja na kuubadilisha uongozi.

Hata hivyo bado haijulikani ni kwa kiwango gani shughuli kubwa za kampuni hiyo zitaathirika katika China bara.

Mwenyekiti wa Kampuni ya ujenzi wa nyumba ya China Evergrande, Xu Jiayin.Picha: Yan Yan/HPIC/picture alliance/dpa

Mkurugenzi mkuu wa Evergrande amesikitishwa na hukumu iliyotolewa lakini anadhamiria kuendelea na shughuli za kampuni.

Hukumu iliyotolewa na mahakama inazingatiwa kuwa kipimo iwapo itatambuliwa China bara.

Soma pia:China yaonya dhidi ya kutanuka mzozo wa mashariki ya kati

Sheria zinazotumika Hong Kong ambazo ni mabaki ya ukoloni wa Uingereza, baada ya Hongkong kurejeshwa kwa China, zinatambuliwa na wakopeshaji kutoka nje inapohusu malipo ya madeni katika China bara.

Hata hivyo China ilikubali kutambua amri za muflisi kwenye miji yake ya Shenzhen, Shanghai na Xiamen.

Hadi sasa mahakama za China bara zimetambua hukumu moja tu juu ya muflisi na China inayo uwezo wa kuamua iwapo kuzitambua hukumu hizo.

China ilitarajiwa wiki iliyopita kuikabidhi kampuni ya Evergrande kwa mahakama ili ifilisiwe na mali zake ziuzwe kwa ajili ya kulipa madeni yake.

Maafisa wa muflisi wanaweza kupendekeza mpango mwingine wa ulipaji wa madeni iwapo kampuni hiyo inazo mali za kutosha na pia wanaweza kuchunguza nyendo zake za ndani, ni kuripoti tuhuma za hitilafu kwa waendesha mashtaka wa Hong Kong.

Madhara ya kutekelezwa kwa hukumu hiyo kiuchumi

Ikiwa kampuni hiyo hatimaye itafilisiwa, hali hiyo itakuwa pigo kubwa kwa mali zake, ndani ya China bara, kwa kutambua kwamba China inashika nafasi ya pili kwa nguvu za kiuchumi duniani.

China bado inakabiliana na atharizilizosababishwa na janga la maambukizi ya virusi vya corona.

China ilitekeleza sera kamilifu ya kupambana na maambukizi kwa kuifunga nchi nzima chini ya karantini.

Tanzania na China zasaini hati 15 za makubaliano

01:19

This browser does not support the video element.

Sekta ya ujenzi wa nyumba wakati wote imekuwa injini madhubuti ya ustawi wa uchumi, mnamo miongo miwili  iliyopita. Kutokana na sekta hiyo China imekuwa inastawi kwa asilimia zaidi ya 10.

Soma pia:Korea kaskazini na China zakubaliana kulinda maslahi ya pamoja

Uchumi wa China ulistawi kwa asilimia 5.3 tu mwaka uliopita kutokana na mauzo hafifu ya nje na utashi mdogo wa ndani na ukosefu mkubwa wa ajira miongoni mwa vijana na pia kutokana na mgogoro katika sekta ya ujenzi wa nyumba.

Mwaka uliopita mauzo ya nyumba mpya yalipungua kwa zaidi ya thuluthi moja.

Serikali za mitaa zinazotegemea mapato kutoka kwenye sekta ya nyumba ili kuongeza bajeti zao sasa zina madeni makubwa na zimelazimika kubana matumizi.

Fungu kubwa la deni la dola bilioni 300 la kampuni ya Evergrande ni fedha zilizolipwa na wananchi wa kawaida.

Sasa haijukulikani iwapo wananchi hao watapewa kipaumbelea katika mchakato wa muflisi.