Miaka 20 jela kwa Rais wa zamani wa Korea Kusini
14 Januari 2021Matangazo
Mahakama hiyo imesema inakataa rufaa iliyowasilishwa na waendesha mashitaka dhidi ya muda uliopunguzwa wa adhabu ya kifungo gerezani uliotolewa mwezi Julai.
Hukumu hiyo inahitimisha uamuzi wa mwisho wa mashitaka ya ufisadi dhidi ya rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 68.
Park anashitakiwa kwa makosa ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka, sambamba na hongo katika mashitaka mengine kufuatia kashfa ya mwaka 2017 iliyosababisha kuondolewa madarakni.
Park ambaye ni binti wa dikteta wa kijeshi Park Chung Hee, aliondolewa madarakani kufuatia wiki kadhaa za maandamano yaliyomtaka ajiuzulu. Kiongozi huyo mara zote amekana mashitaka dhidi yake akisema anaandamwa kisiasa.