1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na Haki

Kifungu cha 42.7: Je, EU inalazimika kujilinda kwa pamoja?

Dotto Bulendu
11 Februari 2026

Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zina wajibu wa kisheria wa kusaidia pande zote chini ya Kifungu cha 42.7 cha mikataba ya umoja huo. Lakini je, nchi ziko tayari kuheshimu ahadi hiyo iwapo kutatokea shambulizi?

Picha ya pamoja I Rais Donald Trump - Greenland
Kauli tata za Rais wa Marekani Donald Trump kuanzia za ushuru wa adhabu hadi azma ya kukinunua kisiwa cha Greenland ziumeibua mjadala mpya kuhusu mkakati wa ulinzi wa Ulaya.Picha: Federico Parra/Odd Andersen/AFP

Mwendelezo wa kauli tata za Rais wa Marekani Donald Trump zikiwemo kuhusu ushuru wa adhabu hadi madai ya umiliki wa kisiwa cha Greenland ziumeibua mjadala mpya kuhusu mkakati wa ulinzi wa Ulaya ambapo wanadiplomasia, maafisa na wataalamu wakifungu cha Mkataba wa Jumuiya ya Kijeshi ya NATO kuhusu iwapo nchi moja mwananchama ikishambuliwa basi ni sawa na shambulio dhidi ya wote.

Kwa muda mrefu, ulinzi wa Ulaya umejikita zaidi ndani ya NATO, muungano wa kijeshi unaoongozwa kwa kiasi kikubwa na Marekani. Lakini kauli za hivi karibuni kutoka kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, zimewafanya viongozi wa Ulaya kujiuliza kama kweli  Marekani bado ni mshirika wa kuaminika katika masuala ya ulinzi.

Mbali na NATO, Kifungu cha 42.7 cha Mkataba wa Lisbon cha ulinzi ndani ya Umoja wa Ulaya kinazitaka nchi wanachama kutoa msaada  kwa njia zote zilizo katika uwezo wao iwapo nchi moja itashambuliwa kijeshi.

Kifungu cha 42.7 cha Mkataba wa Lisbon cha ulinzi ndani ya Umoja wa Ulaya kinazitaka nchi wanachama kusaia kwa namna yoyote ile ikiwa nchi moja itashambuliwa kijeshi.Picha: Jacek Turczyk/dpa/picture alliance

Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya usalama, kifungu hiki kina uzito mkubwa kisheria kinachotoa wigo mpana wa  msaada ndani ya Jumuiya ya Ulaya kwa kueleza kuwa msaada hauishii kwenye silaha pekee, bali unaweza kuwa wa kidiplomasia, kifedha au kibinadam ambapo hata nchi zisizoegemea upande wowote kijeshi, kama Austria au Ireland nazo zinaweza kushiriki kwa namna hiyo.

Hata hivyo wachambuzi  wanasema  kifungu hiki kinachangamoto kubwa kutokana na kuwahi  kutumika mara moja tu mnamo mwaka 2015, baada ya mashambulizi ya kigaidi nchini Ufaransa. Na hata wakati huo, msaada mwingi ulitolewa kupitia muungano mpana unaoongozwa na Marekani.

Kristian Klinck, aliyewahi kuwa mbunge wa Ujerumani kutoka Chama cha (SPD) na mtaalamu wa sera za ulinzi aliiambia DW kuwa anaamini kuwa Kifungu cha 42.7 cha EU ni chenye nguvu zaidi kuliko Kifungu cha 5 cha NATO angalau kwa maandishi. Sharti la kutoa msaada kwa njia zote zilizo katika uwezo wao  lilitafsiriwa kwa upana kumaanisha hadi mwisho wa uwezo wa mtu.

NATO ni nini?

02:15

This browser does not support the video element.

Kifungu hicho kinafafanua zaidi kuwa wajibu huo hautahatarisha au kubadili tabia maalum ya za baadhi ya nchi wanachama ikiwa ni kutambua kwamba kwa baadhi ya nchi, ahadi zao kuu za ulinzi zinaundwa zaidi na NATO

Kwa upande wake Juraj Majcin, mchambuzi wa sera za usalama na ulinzi katika Kituo cha Sera za Ulaya kilichoko Brussels, aliiambia DW kuwa tofauti kuu kati ya vifungu vya ulinzi wa EU na NATO iko katika namna msaada wa ulinzi unavyotolewa. Wakati kifungu cha EU kinategemea zaidi ushirikiano wa kiserikali na misaada ya pande mbili, kifungu cha NATO cha ulinzi wa pamoja kinawakilisha kanuni pana na ya kimuundo ya kuzuia mashambulio

Tangu vita vya Ukraine kuanza mwaka 2022, nchi nyingi wanachama wa jumuiya ya Ulaya zimeongeza bajeti za ulinzi na kuanza kuunganisha mifumo yao ya kijeshi. Ambapo wengi wanautazama Ushirikiano kati ya Ujerumani na Uholanzi, au Ubelgiji na Uholanzi katika jeshi la majini kama  hatua za kuelekea ulinzi wa pamoja wa Ulaya.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW