1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI : Homa ya mafua ya ndege kugubika mkutano wa Rwanda

31 Oktoba 2005

Zaidi ya mawaziri 80 wa serikali za Afrika na wataalamu wa magonjwa ya wanyama leo wanatazamiwa kukutana mjini Kigali Rwanda kwa mkutano wa magonjwa ya wanyama uliotiwa kiwingu na hofu inayoongezeka kwa kuzuka kwa homa ya mafua ya ndege barani humo.

Wakati mada ya mkutano huo wa wiki moja ina mambo mengi kuzuwiya kuingia kwa kirusi cha mafua hayo ya ndege barani Afrika na jinsi ya kukabiliana na taathira za mlipuko wa ugonjwa huo kutapewa umihumu mkubwa.

Mkutano huo awali ulikuwa umekusudiwa kuwa kikao cha kuzungumzia utomokezaji wa sotoka kutoka bara hilo na kuzuwiya kuenea kwa magonjwa mengine ya wanyama kama vile ya kwato na mdomo pamoja na homa ya nguruwe ya Afrika.

Mapema mwezi huu Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema Afrika na jumuiya ya kimataifa itabidi zifanye kila jitihada kuhakikisha kwamba homa ya mafua ya ndege haienei.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW