1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kigali. Jenerali wa jeshi akamatwa katika mahakama za gacaca.

6 Septemba 2005

Mahakama ya kienyeji nchini Rwanda ambayo imekuwa ikiwahukumu watuhumiwa wa mauaji ya halaiki imemkamata jenerali wa jeshi na inasubiri kumhukumu kwa tuhuma za kushiriki katika mauaji hayo mwaka 1994, lakini atapelekwa katika mahakama za kijeshi.

Laurent Munyakazi , afisa wa kwanza wa ngazi za juu wa jeshi kuweza kukamatwa na moja kati ya mahakama hizo za kienyeji ambazo zinajulikana kama Gacaca, alikamatwa Jumatatu katika mji mkuu wa wilaya ya Rugenge na atafikishwa katika mahakama ya kijeshi katika tarehe ambayo haikutajwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW