1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI : Kagame akaripia un’gan’ganiaji madaraka Afrika

11 Septemba 2006

Rais Paul Kagame wa Rwanda amewakaripia viongozi wa Afrika wanaotaka kubadili katiba ili kuweza kuendelea kubakia madarakani kwa kusema kwamba hatua hizo zinatowa picha mbaya ya bara hilo.

Kagame amesema suala hilo linazidi kuwa tatizo kubwa ambalo husababisha taathira mbaya sana kwa nchi zao na kwamba mambo hayo hayafai na yanapaswa kuzuiliwa.Amesema kila kitu kwenye katiba kinaweza kubadilishwa lakini sio vikomo kwa vipindi vya urais madarakani.

Licha ya yeye mwenyewe kudhibiti madaraka kwa muda mrefu nchini mwake kufuatia mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 Kagame anawapinga viongozi watangulizi wenzake wa Afrika kama vile Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Idriss Deby wa Chad ambao wote wawili wameongeza muda wa kubakia madarakani baada ya kubadilisha katiba.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW