1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI : Mahkama Kuu kusikiliza rufaa ya Bizimungu

13 Agosti 2005

Mahkama Kuu ya Rwanda itasikiliza rufaani ya rais wa zamani wa nchi hiyo Pasteur Bizimungu anayeshtakiwa kwa rushwa na uchochezi katika taifa hilo lililokumbwa na mauaji ya halaiki.

Mahkama ya rufaa nchini humo iliamuwa hapo mwezi wa April mwaka huu kwamba haiwezi kuhukumu kesi hiyo ya Bizimungu na hiyo kuipeleka kwa Mahkama Kuu ambacho ni chombo cha juu kabisa cha sheria nchini humo.

Bizimungu ambaye amekuwa gerezani tokea mwezi wa April mwaka 2002 alikutikana na hatia na mahkama ya chini hapo mwezi wa Juni mwaka 2004 kwa ubadhirifu wa fedha za umma, kuchochea uasi wa kiraia na kujihusisha na uhalifu hasa kwa kuanzisha chama cha kisiasa ambacho serikali inakishutumu kwa kutaka kutenganisha watu kwa misingi ya ukabila.

Alihukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW