1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI: Mkutano uanendelea wa kutafuta utatuzi wa mizozo barani Afrika.

16 Machi 2005

Mkutano wa siku tatu unaowajumuisha wabunge kutoka mataifa ya ukanda wa maziwa makuu na pembe ya Afrika unaendelea mjini Kigali Rwanda.

Mkutano huo unaowashirikisha wabunge wanao husika na mashauri ya nchi za nje katika nchi zao unajadili kwa undani jinsi wabunge hao wanavyoweza kuchangia katika utatuzi wa migogoro inayolikumba eneo la maziwa makuu na pembe ya Afrika.

Wabunge hao wanatoka nchi nane za maeneo hayo pia wanajadili mikakati ya utatuzi wa mizozo ya vita na hali ya usalama katika nchi za Afrika.

Akizungumza na wabunge hao rais wa Rwanda Paul Kagame amewaeleza wabunge hao kuwa matatizo yanayowakabili waafrika hayana budi kutatuliwa na waafrika wenyewe.

Amesema chanzo kikubwa cha mizozo katika eneo hilo ni wanamgambo wa kikundi cha Intarahamwe ambao wana maskani yao nchini Congo ambao wanaeneza chuki iliyosababisha mauaji ya halaki ya watu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW