1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI : Mkutano wa kurudishwa wakimbizi leo hii

18 Julai 2005

Maafisa wa Umoja wa Mataifa,Rwanda na Uganda watakutana mjini Kampala leo hii kujadili kurudishwa nyumbani kwa zaidi ya Wanyarawanda 1,100 walioikimbia nchi yao hapo mwezi wa Machi mwaka huu.

Uganda imegoma kuwapa hadhi ya wakimbizi Wanyarwanda 1,169 walioikimbia nchi yao hapo mwezi wa Machi kwa hofu ya kufikishwa mbele ya mahkama za jadi nchini humo zinazowashtaki watuhumiwa waliohusika na mauaji ya halaiki ya mwaka 1994.

Waziri wa serikali za mitaa nchini Rwanda Protais Musoni amesema mkutano huo utafanyika leo hii kati ya serikali za Rwanda, Uganda na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR kujadili hali hiyo na kuandaa mpango wa kuwarudisha nyumbani Wanyarwanda hao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW