1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI : Mmisheni wa Ubelgiji afikishwa mbele ya Gacaca

11 Septemba 2005

Mmisheni wa Ubeligiji amejitokeza mbele ya mahkama za jadi nchini Rwanda na kukanusha kwamba maandishi yake yalisaidia kuchochea mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 ambapo kwayo watu laki nane waliuwawa.

Guy Theunis wa Missionari ya Afrika alifikishwa mbele ya mahkama hizo zinazojulikana kama Gacaca kwa ajili ya kuhojiwa kabla ya jopo la mahakimu kuamuwa iwapo kuwasilisha mashtaka dhidi yake.Thuenis ambaye alifanya kazi kama mhariri wa jarida la la Rwanda la Le Dialogue amekanusha madai kwamba alikuwa akizitowa upya makala ambazo zilichochea mauaji ya watu wa kabila la Watutsi walio wachache nchini Rwanda.

Huyo ni mgeni wa kwanza kufikishwa mbele ya mahkama za Gacaca ambazo zilianzishwa kuchunguza na kuwahukumu zaidi ya watu 760,000 wanaotuhumiwa kuwa na dhima katika mauaji ya halaiki nchini humo hapo mwaka 1994.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW