1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI: Padri wa kikatoliki afikishwa mahakamani

12 Septemba 2005

Padri wa kikatoliki amefikishwa mahakamani nchini Rwanda kwa mashtaka ya kusaidia kuchochea mauaji ya halaiki kiasi ya miaka kumi ya nyuma.Padri Guy Theunis alie Mbeligiji,amekanusha madai kwamba alipokuwa mhariri wa jarida,alichapisha makala yaliyochochea mauaji.Waziri wa mambo ya kigeni wa Ubeligiji,Karel de Gucht amesema kuwa amestajabu kusikia habari za kukamatwa kwa Theunis na ameitaka Rwanda itowe maelezo kuhusu tukio hilo.Theunis alikuwa akifanya kazi kama mmsionari kwa miaka 25 nchini Rwanda,koloni la zamani la Ubeligiji.Kiasi ya watu 800,000 walipoteza maisha yao katika mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW